Top Stories

Binti wa Rais Putin wa Urusi amepewa chanjo ya corona

on

Urusi imeanza uzalishaji wa chanjo mpya ya ugonjwa COVID-19, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la habari la Interfax, likinukuu Wizara ya Afya ya Urusi.
Urusi inasema chanjo hiyo iliyogunduliwa na taasisi ya Gamaleya na kuwa ya kwanza kutengenezwa, itazinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.
August 11 2020, Rais Vladmir Putin wa Russia alitangaza kuwa, nchi yake imegundua chanjo ya kwanza kabisa ya virusi vya corona inayotoa kinga ya kudumu dhidi ya virusi hivyo.

Putin amesema kuwa tayari binti yake mmoja amepewa chanjo hiyo inayozuia maambukizi ya virusi vya corona na maradhi ya COVID-19.

Zaidi ya watu 21,385,925 wameambukizwa virusi vya corona kote duniani. Marekani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika na watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo.

WAZIRI “HUYO MWANAMKE ASIKANYAGE HAPA, TUKIPEWA MAJUKUMU MAKUBWA TUNABORONGA”

Soma na hizi

Tupia Comments