Top Stories

Corona yasababisha Benki Kuu kushusha riba na amana (+video)

on

Benki kuu ya Tanzania imeshusha kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa na benki za kibiashara kutoka asilimia 7 mpaka asilimia 6 ili kukabiliana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa ya virusi vya CORONA katika uchumi

Akitoa taarifa hiyo jijini DSM Gavana wa benki kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema zaidi ya kushusha amana pia kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki kukopa benki kuu kimepunguzwa kutoka asilimia 7 hadi asilimia tano ili mabenki kukopa benki kuu kwa riba nafuu hivyo kupunguza riba za mikopo kwa wateja wao.

Soma na hizi

Tupia Comments