Lazima upige hesabu za harakaharaka ukisikia mtu kahukumiwa kwenda jela miaka 30, ni umbali mrefu sana ambao inaweza kukuchukua muda kuitafakari hiyo safari.
Habari zilizoingia mchana huu kutoka Bukoba Kagera Tanzania ni kwamba Mahakama ya Wilaya Bukoba kupitia kwa Hakimu Mkazi Joseph Luambano imemuhukumu Emanuel Cleophace (20) kwenda jela kwa miaka 30 kwa kosa la kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha nne.
Mwanafunzi alieolewa alikua akisoma kwenye Shule ya Sekondari Kabugaro iliyopo kwenye Manispaa ya Bukoba Kagera ambapo Mawakili wa Serikali Emmanuel Kahigi na Haruna Shomary walikua wakiisimamia kesi hiyo toka mwaka 2016 na Hukumu imetolewa leo.
Mtuhumiwa ni mkazi wa Bukoba na alikuwa akikabiliwa na kosa la kumuoa Adilia Alistides mwenye umri wa miaka 18 ambae wakati anamuoa alikua amehitimu kidato cha nne lakini matokeo yalikua bado hayajatoka
Tazama zaidi hii video hapa chini kujionea
MAGAZETI LIVE!! JPM 2018 ITAPENDEZA…. POLISI WAGONGA MWAMBA KUMUHOJI LISSU… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA