Stori Kubwa

Picha za mtoto wa Whitney Houston akiwa kwenye jeneza ni biashara? familia je?..

on

krt

Bobbi Kristina amefariki akiwa na miaka 22 baada ya kuugua muda mrefu kutokana na kudondoka bafuni..sababu ikidaiwa ni kuzidiwa na dawa za kulevya alizokua akitumia.

August 3 ilikuwa siku ya mazishi yake,  baada ya kumalizika familia yake imeamua kuuza picha za marehemu Bobbi Kristina akiwa ndani ya jeneza kwa dola 100,000 sawa na zaidi ya 200,000,000 za Kitanzania.

fu

Uamuzi wa familia yake ni mwendelezo kwani mama yake mzazi marehemu Whitney Houston naye picha zake zilikua zikiuzwa na kuchapishwa na watu maalum kutoka Makumbusho ya Taifa.

baba

Wakati wa kuandaa mazishi yake familia ya Houston ilikua makini sana kuhakikisha picha za marehemu mtoto wao akiwa ndani ya jeneza hazivuji huku Shangazi yake Bobbi Kristina aitwaye Leolah Brown akisimamia kazi hiyo.

kbbb

Bobbi Kristina amezikwa pembeni ya kaburi la mama yake Whitney Houston August 3 katika makaburi ya Westfield yaliyopo New Jersey, Marekani.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments