Burudani

Black Panther kutoka Julai 8 bila Chadwick Boseman

on

Tayari imetimia miaka mitatu tangu itoke ile filamu iliyovunja rekodi kadhaa za mauzo duniani na kuchukua hisia za watu wengi ya ‘Black Panther’, good news ni kuwa, uzalishaji wa filamu hiyo ya pili itakayoitwa “Black Panther Wakanda Forever” umeanza rasmi mjini Atlanta.

Kwa mujibu wa Jarida la ‘Variety’, Mkuu wa uzalishaji wa studio za uzalishaji filamu za Marvel, Kevin Fiege, amesema kuwa uzalishaji wa filamu ya Black Panther Wakanda Forever umeanza tokea Jumanne hii na kuwa licha ya kutokuwepo msanii Chadwick Boseman aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa ya utumbo, washiriki wengine karibia wote wa Black Panther ya kwanza watakuwepo.

“Ni kweli inaleta machungu bila uwepo wa Chadwick Boseman, lakini kila mmoja wetu yuko tayari kuurudisha Ulimwengu wa Wakanda mbele ya Umma tena na mbele ya mashabiki, tunakwenda kuitengeneza filamu hii kwa namna ambayo ingemfanya Chad ajivunie zaidi” Kevin Fiege.

Filamu hiyo ambayo inamrudisha tena Director Ryan Coogler aliyeongoza Black Panther ya kwanza, inatarajiwa kutoka Julai 8, 2022.

MZEE AFUNGUKA KWA HISIA MBELE YA DC GONDWE “HATUKUTAKA KUJA HAPA, NASI TUNASHUKA HUKOHUKO”

Soma na hizi

Tupia Comments