April 10, 2017 imenifikia hii stori ya jengo lenye uzito mkubwa zaidi ambapo unaambiwa Jengo la Bunge la Romania lina uzito unaotajwa kufikia 4,098,500,000 kg na kulifanya kuwa jengo lenye uzito mkubwa zaidi duniani.
Jengo hilo lipo katika mji wa Bucharest, pia linajulikana kama House of the Republic au People’s House, ni moja kati ya majengo yenye utata Romania kutokana na historia yake likiwakilisha moja ya majengo ya anasa na yaliyotumia gharama kubwa katika historia ya binadamu.
People’s House ni jengo la utawala la pili kwa ukumbwa duniani nyuma ya Pentagon lililopo Marekani kwa eneo na jengo la utawala zito zaidi duniani linalotumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo pia Makao Makuu ya Southeast European Corporative Initiative (SECI) na kivutio cha utalii.
Jengo hili lina urefu wa futi 275.6 na linatawala eneo la square mile 1.41 na ujazo wa cubic meter 2.55 million likiwa na uzito wa 9.04 billion pounds (kilo 4,098,500,000) na lilitajwa kuwa na thamani ya Dollar 3.4 billion mwaka 2008 na kulifanya kuwa jengo la utawala ghali zaidi duniani.
Kwa namna lilivyojengwa lina vyumba 1,100, lakini vilivyokamilika hadi sasa ni vyumba 400 vilivyojengwa kwa Roman style huku miongoni mwa vitu ambavyo vinavutia sana katika jengo hilo ni uwepo wa milango iliyowekwa kwenye Ukumbi wa Nicolae Balcescu ambayo ilikuwa zawadi kutoka kwa Mobutu Sese Seko, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo).
AyoTV MAGAZETI: Ulikosa kilichoandikwa kwenye magazeti ya April 10, 2017? Bonyeza play kutazama.