Dunia ya sasa ni dunia iliyotawaliwa na teknolojia na mitandao ya kijamii imechukua nafasi kubwa kwenye maisha ya kila siku ya Watu wengi duniani na kurahisisha mawasiliano na kuwaweka pamoja hata Watu ambao hawajawahi kukutana ambapo kila mmoja ana tabia zake huko alikotoka.
Kitendo cha Mitandao kuleta huo urahisi wa mawasiliano tumeshuhudia jinsi ambavyo sasa hivi imekua rahisi Mtu kumuandikia Mtu mwingine iwe ni kwa nia nzuri au mbaya na wengine hufikia mpaka kugombana na kurushiana maneno baada ya kupishana, sasa leo nimekuletea majibu ya utafiti kuhusu kujibizana mitandaoni.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Bernstein uliochapishwa kwenye The wall street Journal unaeleza kuwa kuonesha hasira mtandaoni pale unapokutana na meseji au comment ya kukukera hakukusaidii zaidi ya kukuongezea tu hasira nyingine.
“Unapokutana na jambo la kukera mtandaoni kuanza kujibu kwa hasira na wewe ukijibu mashambulizi hakuna faida, busara unayopaswa kuifanya ni kuzima computer au simu kwa muda hadi hasira ziishe na vilevile unaweza kum-block Mtu aliyekukera kwa muda ili usipate ushawishi wa kumjibu” – utafiti huo umeeleza.