Ad

Mix

Kama umepata taarifa ya msiba wa msanii Bongo Movie, ukweli niliothibitishiwa ni huu !!

on

Baadhi ya wasanii walipost mitandaoni wakitoa taarifa ya msiba wa msanii wa Bongo Movie, jitihada zangu zimefanikisha kumpata msemaji wa shirikisho la wasanii Tanzania ambapo kanithibitishia kinachoendelea nyumbani kwa mtoto wa mama huyo, Bagamoyo.

Taarifa ya msiba ilisambazwa hivi >>> “Alipigiwa simu Rais wa Shirikisho la filamu na watu wa Bagamoyo ambao ni majirani zake, baadhi ya watu anaofanya nao kazi pia walithibitisha…. kwa sababu tulikuwa kwenye mkutano ilibidi atangaze.”- Msemaji wa wasanii Tanzania,  Masoud Kaftany

Baada ya kufanya mawasiliano na watu wa lile eneo ambapo walisema kuna msiba, kwa bahati nzuri akapatikana mwanae akasema kwamba mama yuko hai, yuko Hospitalini kalazwa Hospitali ya Bagamoyo ana tatizo la pressure.”-  Masoud Kaftany.

Screenshot_2015-12-04-20-03-51

Mipango ya Bongo Movie kwa sasa ni hii baada ya kuthibitisha kwamba Mama Tecla Mjata hajafariki >>> “Ikifika asubuhi tutajua nini tunafanya ikiwezekana kwenda kumuona Hospitali” >>> Masoud Kaftany.

Hizi ni baadhi ya post za wasanii waliopost taarifa ya msiba.
Screenshot_2015-12-04-20-09-10

Screenshot_2015-12-04-20-09-35

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFB YOUTUBE

Tupia Comments