Mix

Maneno ya Ridhiwani Kikwete baada ya kuona post ya Nape kuhusu Bendera..!

on

Waziri wa Habari,Sanaa,Utamduni na Michezo Nape Nnauye

Kwenye vitu vilivyoleta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Wikiend iliyopita ni pamoja na suala la Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Nape Nnauye kumkabidhi Bendera ya Taifa, Diamond Platnumz ambaye alikua anaelekea Gabon kwa ajili ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya kombe la Afrika (Afcon 2017).

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete.

Baada ya Diamond kufika Gabon ilipigwa picha ya pamoja na wasanii mbalimbali walioenda kutumbuiza wakiwa na bendera za nchi zao,baada ya picha hiyo Waziri wa Habari Nape kupitia twitter aliandika >>’Ulizeni tena kwanini nilimkabidhi bendera Diamond‘ akamaliza na ki-alama cha kushangaa.

Mara baada ya tukio la kukabidhiwa bendera ya taifa Diamond Platnumz kabla ya kuelekea Gabon,Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aliandika kuhusu kushangazwa na hali hiyo na aliandika >>’TFF nadhani mnajua kuwa Mungu wa Watanzania anawaona.Tumefika hapa baada ya mpira kutushinda kabisa.Sasa tunatoa Bendera kwa wanaokwenda kuburudisha na sio wanamichezo tena……..Ngashindwa mie’.

Kwa sababu mjadala umekua mrefu sana kupitia twitter,baada ya post ya Waziri Nape kwenye watu walioandika tena ni Mbunge Ridhiwani Kikwete na aliandika>>’Nafikiri Waziri amepanik kutokana na mashambulizi lkn ukweli ni kuwa tunahitaji kushiriki afcon 2019′.

Video: Waziri Nape alivyomkabidhi Diamond bendera, anakwenda kutumbuiza Garbon>>>

Tupia Comments