Katika Jimbo la Segerea Dar es salaam kuna zahanati kumi lakini hakuna zahanati hata moja iliyopandishwa hadhi ya kuwa kituo kikubwa cha afya chenye uwezo wa kulaza wagonjwa.
Nakukutanisha na Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akiuliza Swali…>>’Je, Serikali ina mpango gani wa kuipandisha hadhi zahanati ya Tabata ‘A’ kuwa kituo ,cha Afya kwa sababu ina miundombinu yote inayofaa?‘
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Suleiman Jafo kamjibu kwa kusema…>>’Zahanati ya Tabata ‘A’ haina eneo la kutosha kukidhi upanuzi wa miunombinu inayofanyika na hivyo inakosa sifa ya kupandishwa hadhi kuwa kituo cha Afya.‘
‘Ili Zahanati iweze kupandishwa hadhi kuwa kituo cha Afya inatakiwa kuwa na wodi ya wanaume na wanawake zenye vitanda 24 kila moja, jengo la upasuaji, wagonjwa wa nje, huduma za mama na mtoto, chumba cha maiti na kichomea taka‘
‘Kwa kuwa Zahanati ya Segerea ina eneo la kutosha, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetenga shilingi milioni 75.0 katikanajeti ya mwaka 2015/2016 ikiwa ni maandalizi ya kuipandisha hadhi kuwa kituo cha Afya.’
ULIIKOSA Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE