Habari za Mastaa

“Weusi siyo kama bendi ya Dansi” – Bonta

on

Staa wa Bongofleva kutoka kundi la Weusi ambalo limekuwa linafanya vizuri Bonta leo April 13, 2017 kupitia kipindi cha XXL ya Clouds amezungumzia juu ya kutoonekana mara kwa mara kundini.

Bonta haonekani kwenye kundi la WEUSI kama wafanyavyo Nikki wa Pili, Joh makini na Gnako na hajasita kulisemea hilo akisema amekuwa mbali kutokana na majukumu ambayo yanamfaya awe mbali kwenye baadhi ya kazi zinazofanywa na wana kundi.

Bonta ambaye ndiyo CEO wa kampuni ya WEUSI ambayo imesajiliwa kibiashara amesema:>>>”Weusi siyo kama bendi ya Dansi. Nipo mbali nao kimajukumu, thus why nakosekana kwenye kazi nyingi. Mimi ndiyo CEO wa WEUSI Kampuni tumeweza kuisajili kibiashara kabisa na tunaweza tusiwe marafiki kwenye muziki ila ni marafiki kifamilia. Mimi na Joh Makini tumetoka mbali pamoja na Lord Eyez.” – Bonta.

Alipoulizwa kuhusu wimbo wake mpya alioutambulisha leo kupitia kipindi hicho, Bonta alisema:>>>“Ngoma yangu mpya inaitwa Ziro inazungumzia juu ya mfumo mzima wa Elimu; kuanzia elimu ya msingi hadi Chuo na nimerekodi tangu mwaka jana. Sijazungumzia kuhusu mtu mmoja, imezungumzia mfumo na huu ndiyo wakati wake.” – Bonta.

VIDEO: Couples mbili zilizoshinda kwenda Ngorongoro leo

Soma na hizi

Tupia Comments