Top Stories

Bobi Wine apinga matokeo Uganda, ajitangaza mshindi kiti cha urais

on

Mgombea Urais nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama ‘Bob Wine’ amepinga mchakato wa utoaji matokeo wa nafasi hiyo unaoendelea nchini humo.

Taarifa zinabainisha kuwa, matokeo ya awali yanaonesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa wingi wa kura.

Bob Wine kutoka Chama cha National Unity Platform (NUP) anadai uchaguzi huo uliofanyika jana ulitawaliwa na wizi mkubwa ambao haujawahi kutokea katika historia za chaguzi zilizowahi kufanyika nchini humo.

Licha ya Tume ya Uchaguzi nchini humo kuendelea na mchakato wa kuhesabu kura, Bob Wine tayari amejitangaza kuwa yeye ndiye mshindi halali wa kiti hicho.

KIM VITA UPYA AFICHUA MAKOMBORA ALIYOFICHA “MAREKANI ADUI MKUBWA” AMTISHA BIDEN

Soma na hizi

Tupia Comments