AyoTV

Ni kweli Bob junior alikamatwa na kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya saa 20 Magomeni, ( stori kamili ninayo hapa)

on

Ni headlines zilizochukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali kuhusiana na msanii Bob Junior kukamatwa na jeshi la polisi, kilichotokea ni kweli kwamba Bob Junior alikamatwa na Polisi na kushikiliwa kwa zaidi ya saa 20 jijini Dar es salaam.

Nilikuja kukamatwa na askari Polisi hapa studio kwangu na nikaambiwa nimehusika katika ujambazi na nimemteka mtu, nikashangaa sababu ni kitu ambacho kiko tofauti na mimi, nikakamatwa nikapelekwa kituo cha Polisi Magomeni Usalama, nikaulizwa unamjua kijana anaitwa Jumanne? nikajibu hapana‘ – Bob

Kumbe huyu Jumanne alimuaga mke wake kwamba anakwenda kwa Bob Junior na kuanzia hapo hakupatikana hewani kwenye simu na kutojulikana alipo, mke wake Jumanne ambaye anatokea kanda ya ziwa ikabidi aende Polisi kuandika kwamba maelezo Polisi kwamba hajamuona mume wake toka alipoaga kwenda kwa Bob Junior

Polisi ikabidi wanifate mimi sababu ni mtuhumiwa wa kwanza ndio maana nikakamatwa kwenda kutoa maelezo Polisi, kiukweli simfahamu Jumanne japo alimuaga mke wake anakuja kwenye studio yangu kurekodi, baada ya hapo Mama yangu na mpelelezi wa Polisi walikwenda mpaka Tigo kuangalia kama nimewahi kuwasiliana na Jumanne na ikakutwa sijawahi kuwasiliana nae, nikapata dhamana baada ya hapo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, InstagramnaYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments