Maafisa Usafirishaji (Bidaboda) wilayani Nyangh”wale Mkoani Geita wamehaswa kutojiusisha na Vitendo vinavyoweza kupelekea kuvunja amani sambamba na kutojihusisha na Shughuli za kiuharifu .
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Geita , Manjale Magambo wakati alipofanya ziara ya wilayani humo na kugawa Reflecta huku akiwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za Mikopo ya asilimia kumi sambamba na vijana kushiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu 2025.
“Moja ya kundi la muhimu ambalo ni kundi la Bodaboda na sisi tunaifanya kazi hii tukitambua dhamira njema ya mh rais kwenu ninyi na mimi ni mashahidi hata kwenye zile faini za Barabarani zimetoka shilingi 30000 mpaka 10000Mh Rais anatambua kundi hili muhimu na anawapenda sana na moja ya maelekezo yake siku zote anasema tuyafikie makundi haya , ” Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo.
Manjale amesema Kundi la Maafisa wasafirishaji ni kundi muhimu sana kwa serikali ya chama cha mapinduzi huku akiwataka kufuata sheria za Barabarani pindi wanavyokuwa wanaendesha vyombo vyao vya moto .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyang’hwale John Aizack amempongeza Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita kwakuona umhimu wa kufanya ziara ya kutembelea wilaya hiyo pamoja na kulithamini kundi hilo la Maafisa Usafirishaji .
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale Hussen Kasu amesema Kundi la Maafisa wasafirishaji limekuwa kundi muhimu ndani ya wilaya hiyo huku akisema wamekuwa wakiwasaidia sana kuwa sehemu ya kulinda Baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa na changamoto ya vitendo vya kiuharifu