Serikali kwa kushirikiana Mashirika mbalimbali likiwemo shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na Plan International ndani ya Mkoa wa Geita wameendelea kudhibiti Vitendo vya Kikatili kwa Mtoto wa kike ambapo wamekuwa wakianzisha mashindano ya michezo ya mpira kwa kushirikisha Kata mbalimbali ndani ya Mkoa wa Geita.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya mpira katika uwanja wa Kasamwa mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi.Janeth Mode amesema lengo la mashindano hayo kuwakutanisha Bodaboda kwani wamekuwa wakitumika katika Njia mbalimbali katika kumrubuni mtoto wa kike asimalize shule kutokana na lifti za Bodaboda.
“Lengo kubwa la Michezo hii ilikuwa ni Kumsaidia Mtoto wa kike aweze kusoma asiweze kupata Mimba za Utotoni lakini Pia asiweze kuolewa kwa umri ambao haufai kauri yetu mbiu inasema si sawa bila usawa si sawa bila nini ni kwanini tuliamua kuwahusisha vijana wetu wa bodaboda bodaboda ni watu ambao wanatumika katika njia mbalimbali zinaweza zikawa sahihi au zisiwe sahihi, “ Mwakilishi wa Katibu Tawala wilaya Geita.
Sabbato Saimon ni Afisa Mradi wa KAGS kutoka shirika la Plan International Mkoa wa Geita amesema leo wamehitimisha fainali za Mashindano hayo yaliyokutanisha Timu za Bodaboda kutoka Ludete pamoja na Ihanamilo amesema Mradi huo ulilenga kutetea haki ya Mtoto wa Kike kuhakikisha anakamilisha Ndoto yake ya Kimasomo kwani Waendesha Bodaboda wamekuwa wakihisiwa kuwarubuni watoto wa kike hasa wale wanaotoka katika Mazingira Magumu pamoja umbali .
“Kwa siku ya leo tunahitimisha ligi ya Bodaboda ambayo imeanza Mwaka huu mwezi wa kwanza lengo ilikuwa ni kuwaandaa waendesha Bodaboda kama mnavyojua takwimu zinaonesha kwamba waendesha bodaboda wanachangia sana mimba za utotoni na kama sio kumpa Mimba mtoto bhasi anamsafirisha kumpeleka sehemu ambayo ataenda kupatia hiyo Mimba, ” Afisa Mradi KAGS Geita.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo Mkoa wa Geita Ndg.Harun Erikana ametoa shukurani za kipekee kwa namna walivyowaelekeza vijana katika kuratibu kushiriki katika Mashindano hayo ambayo yameshusisha Timu 94 ndani ya Mkoa wa Geita.