Madereva boda boda kutoka Uyole-Mbeya wameingia kwenye headline baada ya kuamua kuondoka na mwili wa marehemu Gabriel Osward Ngalele ambaye alikua pia ni dereva boda boda mwenzao.
Tukio hilo limetokea ndani ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG] Uyole Njia Panda ambapo taarifa inasema kuwa mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo kwa ajili ya ibada.
Marehemu Gabriel Osward Ngalele.
Ibada hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa hilo,wakati ibada ikiendelea Mchungaji aliomba utulivu kwa wafiwa ambao walitulia,Lakini vijana zaidi ya 300 ambao inasemekena ni waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele kanisani hapo.
Hali hiyo ilimfanya mchungaji kuwaomba tena utulivu hata hivyo vijana hao waliendelea kukosa utulivu ndani ya kanisa hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyoibua mtafaruku mkubwa.
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole.
Katika mtafaruku huo ulipelekea vijana hao kuuchukua mwili wa marehemu kwenda nao hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji kanisani,hata hivyo jeshi la polisi lililazimika kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani kwa kumrejesha mchungaji huyo nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.
Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Vicent Mwashoma na ibada ya mazishi kuendeshwa na Bahati Mwasote ambae inadaiwa ni mchungaji wa Bodaboda.
Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote
Taarifa inasema marehemu Gabriel Ngalele alifariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambao wote walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Stori na picha toka:mzalendohuru.blogspot.com