Bodi ya Huduma Za Maktaba Tanzania imeandaa kongamano la Pili la kitaifa la Huduma za Maktaba Tamasha la vitabu na usomaji litakalofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 Bodi yaNovemba mpaka tarehe 24 Novemba mwaka huu Mkoani Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt Mboni Ruzegea amesema lengo la Kongamano hilo ni kutoa fursa kwa wadau wote wa huduma za maktaba nchini kushiriki, kuchangia na kuamua kwa pamoja namna bora ya kuendesha huduma za maktaba nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Pia Mkurugenzi amesema kuwa kwenye kongamano hilo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Pia ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kuona maktaba kwa Jicho la pekee na kuzifanyia karabati maktaba 7 za hapa nchini ili kufufua na kuboresha elimi nchini kupitia huduma za maktaba.