Michezo

Bodi ya Ligi ya ufungia uwanja wa Sokoine

on

Bodi ya ligi Kuu Tanzania imeafikia maamuzi ya kuufungia uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kuchezewa kwa mechi zozote za mashindano.

Uwanja huo umefungiwa kuanzia leo Desemba 26 2019 kutokana na kuharibika sana sehemu ya kuchezea (pitch) baada ya tamasha la wasanii kufanyika katika uwanja huo siku ya Christmass kitu kilichopeleka kuharibika kwa kukanyagwa kwa nyasi za uwanj huo.

Timu za Ligi kuu, daraja la kwanza (FDL) na ligi daraja la pili (SDL) zilizokuwa zinatumia uwanja huo kama wa nyumbani au kituo chake basi zimeagizwa kutafuta uwanja mwingine wa kutumia hata mchezo wa Prisons na Yanga uliokuwa unapangwa kucheza hapo December 27 hauwezi tena kuchezwa.

Soma na hizi

Tupia Comments