Habari za Mastaa

Hii ndio idadi ya Movies zilizopokelewa na Bodi ya Filamu Tanzania kuanzia mwaka 2014/2015

on

.

.

Inawezekana ukawa na hamu ya kufahamu ni idadi ngapi ya movie zinazopitishwa ambazo zimefanyiwa marekebisho na kufaa kimadili, sasa leo nakukutanisha na Bodi ya Tanzania ambao huwa wanahusika kuzipokea filamu zote za Tanzania na kuzipitisha.

Akizungumza kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM, Bi. Joyce Fisso Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania alisema;..”kati ya filamu 447 , filamu 47 zilihitaji marekebisho na  tunaposema marekebisho kwamba ni kuna vipengele ambavyo tunaona vinaweza kurekebishika na visiharibu hadithi lakini vile vile visikizane na sheria yetu na bahati nzuri wadau wetu wote wamerekebisha na kurejesha

Millardayo:..’Sasa hivi kwa Tanzania mnapokea filamu ngapi kwa mwezi?…”

Bi.Joyce:..’Kwa mwezi tunapokea kati ya filamu 40 mpaka 100, lakini kati ya Julai mpaka mwaka huu  sasa tumeshapokea filamu 447 kwa maana ya majina lakini kama unavyojua filamu zetu nyingi ni part 1 na part 2  kwa hiyo kati hizo za part 1 na part 2 ni zaidi  ya 660..

Unaweza uka bonyeza play kusikiliza interview hapa

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

 

Tupia Comments