Mix

Jeshi la Nigeria limewakamata hawa wengine waliojihusisha na Boko Haram!

on

Headlines za Boko Haram zinaendelea kusikika, ni kama vile wanapumzika kidogo alafu wanaibuka tena… Mpya kutoka Nigeria leo inawahusu baadhi ya watu waliokamatwa na Jeshi la Nigeria kwa mashtaka ya kuwa wao ndio waliokuwa wanahusika kupeleka mafuta ya petroli na bangi kwenye maficho ya Boko Haram.

supplier1

Baadhi ya watu waliokamatwa wakijihusisha na vitendo vya kigaidi na Boko Haram.

Mkurugenzi wa Jeshi Mahusiano ya Umma Nigeria, Sani Usman alitoa kauli hiyo kupitia mtandao uitwao Prompt News Online, na kusema…

>>> ” Waalifu hawa ndio waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kupeleka mafuta ya petroli, bangi na vilevi vingine … Jeshi la Nigeria litaendelea kupambana kadri liwezavyo dhidi ya vitendo vya kigaidi kwenye nchi hii ili kuhakikisha Nigeria inabaki salama na yenye amani… Lakini hivi vyote vitakuwa vigumu kutimiza kama hatutakuwa na ushirikiano kutoka kwa umma, tunakaribisha taarifa yoyote ile dhidi ya matukio au mipango ya Boko Haram inayoendelea kwenye jamii “. <<<  Sani Usman.

Supplier-2

Baadhi ya vitu vilivyokamatwa kwenye camp ya Boko Haram.

Mkurugenzi wa Jeshi Mahusiano ya Umma, Sani Usman amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao waliokamatwa ambao kwa muda mrefu wamekuwa kikwazo cha amani sehemu mbalimbali nchini Nigeria kwa kujihusisha na Boko Haram.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments