Mix

Miili 35 ya watu ilivyopatikana baada ya mashambulizi ya Boko Haram Nigeria..

on

Mara ya mwisho kusikia headlines za matukio ya Boko Haram, Nigeria ilikuwa miezi kadhaa iliyopita na eneo la mwisho kusikia Boko Haram wapo lilikuwa Jimbo la Bama… lakini leo kuna headlines mpya kuhusiana na jimbo hilo.

Zaidi ya miili ya maiti 35 iliyofukiwa kwenye maeneo ya jimbo la Bama imegundulika na Serikali ya mtaa miezi minne baada ya Jeshi la Nigeria kufanikiwa kuondoa vikosi vya Boko Haram katika eneo hilo.

Boma2

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa eneo husika, Ali Guija amewaambia waandishi wa habari jana November 26 2015 kuwa maiti hizo zilipatikana kwenye nyumba nyingi zilizoharibiwa na Boko Haram kwenye mashambulizi waliokuwa wakifanya kwenye mitaa ya jimbo hilo.

>>> “Tumefanikiwa kupata maiti zaidi ya 35 kwenye Jimbo la Bama kwenye zoezi la usafi tulilokuwa tunafanya maeneo hayo baada ya kupewa kibali na Serikali kusafisha mitaa ya Jimbo hilo ili kutoa nafasi ya kufanya ukarabati wa nyumba zilizoharibiwa ili watu waweze kurejea makazi yao ya zamani“. <<< Ali Guija.

Boma

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments