Michezo

Bologna wameheshimu uamuzi wa Zlatan kinyonge

on

Mshambuliaji wa zamani wa Man United na LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic hatma yake ya kujulikana atajiunga na timu gani kufahamika hivi karibuni ikiwa ni siku chache zimepita toka athibitishe kuwa anaondoka LA Galaxy na MLS.

Ibrahimovic atabadili timu January 1 baada ya mkataba wake na LA Galaxy kumalizika, akiwa na nafasi ya kusaini timu yoyote bila malipo ya ada ya usajili, club ya Serie A ya Bologna ndio inaonesha dhamira zaidi ya kumshawishi Zlatan arejee tena Italia ila katika club ya Bologna.

Mkurugenzi wa michezo wa Bologna Walter Sabatini amethibitisha kuwa imeshindikana wao kupata uhakika wa kumsajili Zlatan baada ya mchezaji huyo kukataa ofa yao huku akise.a ameshafanya maamuzi mengine ya timu ya kujiunga nayo.

“Hawezi kuja Bologna ameshafanya maamuzi mengine, tumefurahi tu hata kumpendekeza ajiunge zetu, ameshafanya maamuzi mengine ya kiweledi kulingana na mtazamo wake ni kuhusiana pia na mahusiano binafsi kati ta Ibra na Mihajlovi (Kocha Bologna) nasisitiza halikuwa suala la pesa”>>>> Zlatan

Soma na hizi

Tupia Comments