Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) imetangaza April 12, 2024 itaanza zoezi la ubomoaji nyumba katika Bonde la Msimbazi, Jijini Dar es Salaam ili kupisha ujenzi wa daraja, mto, City park na ujenzi maeneo ambayo ni korofi ambapo mradi huo utagharimu dolar za kimarekani milioni 260
Hayo ameyasema Mhandisi Humphrey Kanyenye ambaye ni Mratibu wa miradi ya ushirikiano na Benki ya Dunia (TARURA)
“Tunataka kuanza zoezi la kubomoa pale msimbazi kwa ambao tumeshia walipa wale 2155, tumepanga kuanzia rasmi tarehe 12 April mwaka huu, wakati wa kulipa fidia tulikubaliana wataondoka ndani ya wiki 6, kwa wale ambao wameshindwa kufanya hivyo sisi tuanza hili zoezi tarehe 12”