Ni November 29, 2024 ambapo Benki ya CRDB inazindua SAMIA INFRASTRUCTURE BOND katika Ukumbi wa Mikutano Mlimani City Hall jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa waliozungumza ni Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI.
“Hati Fungani hii ni zaidi ya bidhaa ya kifedha. Ni chombo cha kuhamasisha maendeleo ya haraka na endelevu kupitia Makandarasi wazawa, ambacho kitaharakisha utekelezaji wa miradi ya barabara nchini, kuimarisha uchumi wetu na kuleta manufaa kwa wananchi wote. Tunapozindua hati fungani hii leo, tunashuhudia mwanzo wa mafanikio makubwa kwa Makandarasi Wazawa, kwa wananchi, na kwa taifa letu zima. Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI.
“Lengo kuu la kuanzisha Hati Fungani Hii ya Miundombinu ya Samia (Samia Infrastructure Bond) ni ili kuwasaidia wakandarasi Wazawa kukabiliana na changamoto za kifedha wanazokutana nazo na kuwawezesha kushiriki katika miradi mikubwa ya miundombinu ya barabara.” – Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI.