Michezo

Bondia Hassan Mwakinyo ashika namba 1 Afrika

on

Box Rec imemtaja Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo namba moja kwa bara zima la Afrika na namba 37 Duniani kati ya Mabondia 2,050 kwenye uzani wa Super Welter.

Baada ya taarifa hii Mwakinyo amezungumza na Ayo TV & millardayo.com  na kusema ….“Namshukuru Mungu na Support ya Watanzania wote na Menejimenti yangu, nimefurahi kwakuwa ni sehemu ya kuona kwamba nipo njiani kutimiza ndoto au safari ninayoiwaza kutokana na vikubwa vinavyozidi kutokea, naamini kupanda kwa rank huku kuna vichocheo vingi zikiwemo Dua za wote wanaonitakia kheri”- Hassan Mwakinyo

“Imekuwa sehemu ya faraja kwangu naamini kuwa namba moja Afrika sio kitu kidogo, sio kila Bondia anaweza kufika na pia sio sifa ya mimi kufika ila naamini ni wakati ambao Mungu ametaka nifike kutokana na jitihada na nguvu nilizowekeza katika kazi yangu”- Mwakinyo.

 

Soma na hizi

Tupia Comments