Stori Kubwa

Serikali ya Tanzania imethibitisha mradi wa Treni za juu kama hizi kujengwa Dar hivi karibuni.

on

Screen Shot 2014-05-15 at 4.52.21 PMUmekua ni usafiri mwingine mzuri na wenye starehe yake kama ukipata nafasi ya kuutumia kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza Dubai na kwengineko ambako kuna watu wengine wanategemea sana kuutumia na kuacha magari yao nyumbani na kujikuta wamewahi town na kumaliza shughuli zao manake hamna foleni.

Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa Afrika likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya shilingi BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam.

Screen Shot 2014-05-15 at 4.53.09 PMWaziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’

Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.

Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24’

Screen Shot 2014-05-15 at 4.53.27 PMKazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.

Unapenda chochote kinachonifikia kisikupite? jiunge na mimi twitter kwa kubonyeza HAPA pia facebook na Instagram kwa kubonyeza FB na INSTA ili nikutumie kila kitu, kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi mtu wangu wa nguvu.

Una imani kwamba hili la treni litafanikiwa Tanzania hivi karibuni? utapendelea kutumia usafiri wa treni? nipe maoni yako kwa kuniandikia hapa chini..

Soma na hizi

Tupia Comments