Habari za Mastaa

U-heard leo Soudy Brown kainasa ya Tuesday Kiangala kutoka Bongomovie

on

Mtangazaji Soudy Brown kupitia U-Heard ya XXL ya Clouds FM ametuletea story inayomuhusu muandaaji wa Filamu Tuesday Kiangala anayedaiwa kuwaomba mapenzi waigizaji wa kike ili awape scene za kuigiza.

Inadaiwa kuwa Tuesday ambaye ni C.E.O wa Tuesday Entertainment Ltd anawaomba penzi waigizaji wa kike ili awape scene za kuigiza kwenye Tamthilia wakiwa kwenye kambi Lushoto, Tanga.

Soudy Brown amepiga story na Tuesday Kiangala ili kujua ukweli uko wapi na haya ndiyo majibu yake:>>>”Taarifa siyo za kweli. Hakuna msanii wa Arusha aliyefanyiwa kitu kibaya lakini hata kwenye group dada huyo alikuwa analazimishwa ‘sema, sema’. Ni timu ambayo imekaa baada ya kutoka huku na wengine walipandikizwa japo ni kweli kuna wengine nilikuwa na mahusiano nao.” – Tuesday Kiangala.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story

EXCLUSIVE: Steve RnB afunguka kuhusu ukimya wake, ujio mpya

VIDEO: Vipaji vipya Bongo, kutana na kundi jipya la Saut From East

Soma na hizi

Tupia Comments