Top Stories

Boss Jamii Forum alipa faini Milioni 3 aachiwa huru

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forum, Maxece Mello kulipa faini ya Sh.Mil 3 ama kwenda jela mwaka mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kulizuia Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake.

Pia Mahakama hiyo, imemuachia huru mshitakiwa mwenzake Mickie Mushi baada ya kutotiwa hatiani katika makosa yao.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo upande wa utetezi umedai kuwa utakata rufaa kupinga adhabu hiyo.

Tayari Mello amefanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru.

“MGONJWA WA CORONA ALIHISI KAWEKEWA SUMU” AMEPATIKANA ZANZIBAR AMETOKEA TANGA

Soma na hizi

Tupia Comments