Duniani

Boss wa mgahawa alivyofukuzwa kazi baada ya camera kumnasa akimpiga dereva taxi

on

Siku hizi mambo ya teknolojia yamekuja na vingi sana, usije kujibana sehemu ukafanya jambo lolote la ajabu ukitegemea watu hawakuoni.. inawezekana watu hawakuoni ila camera zinakuona !! Boss wa mgahawa mkubwa Marekani ameikosa kazi kama utani, kisa ni tukio lake kunaswa na camera ndani ya taxi !!

Taxi

Boss huyo alijikuta akipoteza kazi yake baada ya camera ya kwenye gari kumrekodi akimvamia na kumpiga dereva wa taxi California, Marekani… Boss huyo Benjamin Golden alikuwa Boss wa Kampuni ya migahawa ya Taco Bell.

Chanzo cha noma yote ilikuwa ishu ya dereva huyo wa Taxi kumuuliza abiria wake ambaye ndio huyo Boss ampeleke wapi? lakini kwa vile Boss Golden alionekana amelewa, alishindwa kutoka maelekezo kwa dereva wapi anakoenda… baada ya muda kidogo walianza majibizano, alafu Boss huyo akaanza kumpiga… Video ilisambaa mitandaoni na baadae Kampuni yake ikatangaza kumsimamisha kazi.

Video yake hii hapa mwanzo mpaka mwisho wa ishu yenyewe ilivyokuwa ndani ya gari.

https://www.youtube.com/watch?v=djAXIjdoWcc

Kipande kingine hiki hapa cha video ya tukio lenyewe ndani ya taxi.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments