Benki kuu ya Tanzania (BOT) imesema imekusanya kiasi cha Tani mbili za Dhahabu zenye thamani ya Shilingi Bilioni 400 kuanzia Mwezi Oktoba 2024 hii ni baada ya Serikali kuondoa tozo ya ukaguzi pamoja na punguzo ya tozo ya Asilimia mbili ya Mrahaba .
Hayo yameelezwa wakati wa Mafunzo ya Uongezaji thamani kwa wanawake wachimbaji yaliyotolewa na Uongozi wa kiwanda cha uongezaji thamani ya Dhahabu (GGR) kwa kushirikiana na Benki kuu ya Tanzania , Joshua Maganga Afisa kutoka kitengo kinachosimamia fedha za kigeni amesema hamasa ni kubwa inayotolewa na Benki hiyo kwa wachimbaji kuiuzia Benki hiyo dhahabu ukilinganisha na miaka iliyopita.
Meneja wa wakala wa huduma za Serikali kutoka Benki kuu ya Tanzania , Sadiki Nyanzuwa amesema awali wachimbaji wengi walikuwa hawakopesheki kutokana na kukosa dhamana nakwamba sasa Serikali imeamua kuweka nguvu ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu utakaosaidia nchi kupata fedha .
Martine Shigela ni Mkuu wa Mkoa wa Geita akifungua Mafunzo hayo amesema Serikali ya awamu ya sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imejipanga katika kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na Rasilimari zilizopo katika eneo lake ikiwemo wanawake kuwa mstari wa mbele katika kunufaika na sekta ya Uchimbaji Madini na Uongezaji thamani.
” Kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia wanawake 1000 wamepatiwa leseni za uchimbaji na kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutoa leseni zaidi ya 2000 katika eneo la Kigosi ambalo awali lilikua hifadhi ya misitu , ” Mkuu wa Mkoa wa Geita , Martine Shigela.
“Maombi ni mengi leseni 2300 lakini maombi ni zaidi ya 4000 na kwa sasa wapo watakaopata lakini tumewaelekeza kwa eneo lililotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo zipo leseni nyingine zaidi ya 4000 tayari nimewapa maelekezo watangaze leseni hizo ili watu waliokosa waweze kuomba ”Mkuu wa Mkoa wa Geita , ” Martine Shigella.