Top Stories

BOT yapunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki (Video+)

on

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imepunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki kinachotakiwa kuwekwa Benki kuu, hatua hii ni kutoa msukumo mkubwa wa kuongeza kasi ya mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza riba na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hii ni sehemu ya hatua tano za kisera ambazo BOT wamezitaja leo ili pia kuweka mambo sawa kutokana na janga la Corona kuathiri shughuli za kiuchumi.

Gavana wa Benki Kuu Prof. Florens Luoga amesema nafuu hii itatolewa kwa Benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa ambapo Benki itakayonufaika itatakiwa kutoa mikopo kwa sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka.

Hatua nyingine ambayo imechukuliwa na BOT ni pamoja na kulegeza masharti ya usajili wa Mawakala wa Benki ambapo imeondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa Waombaji wa biashara ya Wakala wa Benki na badala yake Waombaji wa biashara ya Wakala wa Benki watatakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho cha Taifa.

Profesa Luoga amesema hatua hii itachangia kuongeza fedha katika Mabenki kutokana na ongezeko la amana na kupunguza riba za mikopo.

Soma na hizi

Tupia Comments