Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: BREAKING: Benki kuu Tanzania yafuta leseni ya Benki ya FBME
Share
Notification Show More
Latest News
Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam
August 8, 2022
Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko
August 8, 2022
Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu
August 8, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 8, 2022
August 8, 2022
International Marathon yaacha historia Zanzibar
August 7, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > BreakingNews > BREAKING: Benki kuu Tanzania yafuta leseni ya Benki ya FBME
BreakingNews

BREAKING: Benki kuu Tanzania yafuta leseni ya Benki ya FBME

May 8, 2017
Share
3 Min Read
SHARE

Taarifa ambayo imetolewa na Benki kuu ya Tanzania leo May 8 2017 imesema mnamo tarehe 24 July 2014 Benki Kuu ya Tanzania iliiweka chini ya usimamizi maalumu (statutory management) FBME Bank Limited (FBME).

Uamuzi huo wa Benki Kuu ulitokana na notisi iliyotolewa July 15 2014 na Taasisi ya Marekani inayopambana na uhalifu wa kifedha “the US Financial Crimes Enforcement Network” kwa kifupi FinCEN, iliyoituhumu FBME kuwa ni taasisi inayojihusisha na biashara ya utakatishaji wa fedha haramu (money laundering) na hatua ya Benki Kuu ya Cyprus kuliweka tawi la FBME lililopo nchini Cyprus chini ya uangalizi maalumu (special administration).

Katika Notisi hiyo FinCEN ilitoa kusudio la kuifungia FBME kutotumia mfumo wa kibenki wa Marekani (US financial system) ambapo tarehe 29 Julai, 2015, FinCEN ilitoa uamuzi wa kuifungia FBME kutumia mfumo wa kibenki wa Marekani.

FBME walifungua kesi huko Marekani (US District Court for the District of Columbia) wakiiomba Mahakama kutengua uamuzi wa FinCEN ambapo hatimaye April 14 2017 Mahakama ilitoa uamuzi ambao unairuhusu FinCEN kuendelea na utekelezaji wa uamuzi wake wa mwisho (Final Rule) ambao unaifungia benki ya FBME kutumia mfumo wa kibenki wa Marekani.

Uamuzi huo wa Mahakama unaongeza athari kwa kiwango kikubwa katika uendeshaji wa FBME kwa kuwa haitaweza tena kufanya miamala ya kibenki ya kimataifa na kupata huduma za mifumo ya kibenki na hivyo itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wateja wake kwa mujibu wa leseni waliyopewa.

Kwa kuzingatia athari zinazotokana na uamuzi wa mwisho wa FinCEN, kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(2)a, 11(3)(i), 61(1) na 41(a) vya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imesimamisha shughuli zote za FBME Bank Limited kufuta leseni yake ya kufanya shughuli za kibenki, kuiweka chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kama mfilisi kuanzia tarehe 8 Mwezi Mei, 2017

Kufuatia Benki Kuu kufuta leseni hiyo kuwa Mfilisi kuanzia tarehe 8 Mei, 2017, taarifa inatolewa kwa wenye amana, wadai na wadaiwa kuwa wawe wavumilivu wakati Mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao.

Mfilisi kwa wakati muafaka atawafahamisha wenye amana, wadai na wadaiwa utaratibu wa malipo wa madai, ulipaji wa madeni na taratibu nyingine zitazohitajika kwa mujibu wa sheria na kwa maelezo ya ziada kuna mawasiliano ya Mkurugenzi, Bodi ya Bima ya Amana kwa anuani ifuatayo:

2 Mtaa wa Mirambo
Benki Kuu Makao Makuu, Ghorofa ya Saba, Mnara wa Kaskazini 11884, Dar Es Salaam
Simu: +255(0)22 2235390
Nukshi: +255(0)22 2234200
Barua Pepe: info@bot.go.tz

VIDEO: Binadamu Mzee zaidi duniani anayepatikana Tanzania, bonyeza play hapa chini kumtazama

VIDEO: Flora Mbasha kaolewa tena, tazama harusi ilivyofungwa kwa kubonyeza PLAY HAPA CHINI

You Might Also Like

International Marathon yaacha historia Zanzibar

Mfahamu Panya Kennedy anayebeba Camera kama Binadamu ‘Anarekodi Matukio vitani’ (video+)

Diwani CHADEMA na wenzake waachiwa kesi ya mauaji

Nickson afikishwa Mahakamani kwa kujifanya Rais Samia

Wentworth Resources kushirikiana na Tanzania agenda ya maendeleo endelevu ya Nishati

TAGGED: breaking, Breaking news, TZA HABARI
Millard Ayo May 8, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Waziri wa afya Ummy Mwalimu kuhusu msiba wa watu 32
Next Article VIDEO: Maamuzi yaliyofanywa na Bunge baada ya msiba wa Arusha
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam
Mix August 8, 2022
Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko
Top Stories August 8, 2022
Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu
Mix August 8, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 8, 2022
Magazeti August 8, 2022

You Might also Like

Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 7, 2022

August 7, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 6, 2022

August 6, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 5, 2022

August 5, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 4, 2022

August 4, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?