Habari za Mastaa

Aliondoka kwa Birdman akarudi kwa Jermaine Dupri & sasa Bow Wow yupo na management hii..!

on

Baada ya kuachana na uongozi wa Young Money Cash Money Music & Management, rapper Shad Moss maarufu kama Bow Wow alisema kuwa alifanya maamuzi hayo sio kwa ubaya ila angependelea kuwa chini ya watu wake waliomkuza kimuziki yani Jermaine Dupri na Snoop Dogg chini ya uongozi wa So So Def Entertainment.

Inaonekana safari ya Bow Wow na maamuzi ya kuchagua management ya kumsimamia bado yanaendelea… nimepita kwenye page ya Instagram ya Bow Wow @shadmoss na nimekutana na picha mbili alizopost rapper huyo ikiwa kama ni breaking news kwa mashabiki wake!

bow

Rapper Bow Wow.

Bow Wow ametangaza rasmi kuhamia management ya rapper na mfanyabiashara P Diddy, Bad Boy Entertainment, na kwenye moja ya picha alizopost Instagram Bow Wow amesema…

>>> “nadhani nimefanya uamuzi sahihi kuungana na big bro… watu wangu @jamescruz1 @bart25 na @eliemaroun15 wameshaweka mambo sawa, na sasa naingia kazini. Nafuraha kutangaza hii ndio management yangu mpya.. kutengeneza hela haitokuwa issue sana. #Badboy #cruzcontrol #Newmangagement #Cirocboys #Caviboys.” <<< @shadmoss.

bowwow

Kuonyesha furaha yake rapper huyo alipost picha ya pili na kusema… >>> ” NEWS: Leo Shad Moss ‘Bow Wow’ ametangaza rasmi kujiunga crew ya Bad Boy Management chini ya P Diddy na James Cruz. Shad Moss ameonekana mwenye furaha akiwa tayari kuyapokea mabadiliko haya mapya….” <<< @shadmoss.

bowwow2

Bow Wow hajaishia hapo ameendelea kusambaza taarifa hiyo kupitia page yake ya Twitter kwa kushare tweet hii kwa mashabiki na dunia nzima…

bowwow3

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments