Mix

BREAKING: Kinachoendelea kuhusu kupigwa mnada nyumba za Lugumi

on

August 20 2017 Kampuni ya Udalali ya Yono ilitangaza kupiga nyumba tatu za kifahari mali za Lugumi Enterprises  Ltd, nyumba moja ipo maeneo ya upanga, Ilala na nyingine mbili zipo eneo la Mbweni Dar es salaam kutokana na mmiliki wake kushindwa kulipa kodi kwa mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’.

Mnada umepangwa kufanyika September 9 2017, sasa Leo September 07 2017, Mkurugenzi Mtendaji, Scolastica Kivera amezungumza na waandishi kuhusu ulipofikia mchakato wa kupiga mnada nyumba hizo ambapo amesema mnada huko palepale.

Soma na hizi

Tupia Comments