Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Brazil, Anvisa, kimetangaza kumzuia mtu anayeshukiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa ya nyani katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Sao Paulo.
Kituo hicho kimesema kupitia taarifa kuwa, abiria aliyekuwepo katika eneo maalum kwenye uwanja huo wa ndege lililotengwa kwa ajili ya watu wanaosubiri kuomba hadhi ya ukimbizi tangu mapema mwezi huu, ameonyesha dalili zinazofanana na ugonjwa wa homa ya nyani.
Hata hivyo haikutoa maelezo juu ya sehemu alikotoka au nchi ya asili ya abiria huyo ambaye baadaye alipelekwa hospitali.
Wizara ya afya nchini Brazil imesema zaidi ya wagonjwa 700 waliothibitishwa kuugua homa ya nyani wameripotiwa kote nchini humo mwaka huu, ingawa hakuna hata mmoja aliyekutwa na aina mpya ya kirusi cha homa ya nyani