Brazil ni nchi ambayo kila mpenda soka anaifahamu kwa kutoa vipaji vingi katika soka, katika mfumo wa uzalishaji wachezaji Brazil ni tofauti kidogo na nchi za Ulaya, asilimia kubwa ya wachezaji wazuri kutokea Brazil ni watu ambao wamejifunzia soka mtaani. Brazil ni nchi yenye idadi ya watu milioni 200 lakini asilimia kubwa ya vijana hupenda kujihusisha na mchezo wa soka. November 9 naomba nikusogezee tabia 5 za wachezaji wengi wa kibrazil ambazo wanatajwa kuwa nazo.
1- Ni aina ya wachezaji ambao hupenda kucheza soka nchini kwao, wachambuzi wengi wa masuala ya soka hupenda kusema kuwa wachezaji wa kibrazil huwa wanaumwa homa ya kupenda nyumbani, kama utakuwa unakumbuka vizuri kabla ya Neymar kujiunga na FC Barcelona kulikuwa na mjadala mrefu sana katika baadhi ya vyombo vya habari ambavyo wanaamini Neymar anapaswa kwenda Ulaya na wengine kusema hata Brazil anaweza kuwa mchezaji bora.
2- Wengi wao hutokea maisha ya mtaani na asilimia kubwa mara wapatapo pesa hupenda kufanya starehe kitu kinachotajwa kuwa ni tabia ya kujisahaulisha matatizo. Baadhi ya mastaa wa Brazil wanaotajwa kupenda starehe ni Ronaldinho Gaucho.
3- Ni watu ambao hupenda kujivunia utamaduni wao na kudumisha aina ya muziki wao wa asili Samba hata tumewahi kuona mara kadhaa wakifunga magoli hupenda kushangilia kwa kucheza staili hiyo ya muziki.
Hii ni video ya Ronaldinho akicheza Samba
https://youtu.be/ArTmKwjU24Q
4- Mchezaji yoyote wa kibrazil aliyetokea mtaani anakuwa na uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira kuliko yule anayekulia katika academy za soka barani Ulaya. Mfano mzuri ni Ronaldinho Gaucho ambaye anasifika kwa ufundi na uwezo wake mkubwa wa kucheza na mpira katikati ya msitu wa watu bila kuupoteza.
5- Hata wapate mafanikio kiasi gani utajiri mkubwa vipi majumba na magari ya kifahari usitegemee baada ya kustaafu utaona wanaamua kuweka makazi ya kudumu barani Ulaya, wengi wao ni lazima warudi kwao Brazil na Ulaya kwenda kutembea tu tofauti na baadhi ya wachezaji wengi wa kiafrika ambao hupenda kuweka makazi ya kudumu Ufaransa, hizi ndio sifa na tabia walizonazo wachezaji wengi wa Kibrazil.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.