Habari za Mastaa

Good news: Wimbo wa Diamond & Davido ‘number 1 rmx’ umefika mpaka hapa Brazil

on

Screen Shot 2014-05-09 at 2.14.24 AMZilipita headlines nyingi za Diamond kufanya kolabo na mastaa wakubwa wa muziki Afrika akiwemo Davido na Iyanya, video zake kuchezwa kwenye tv za kimataifa na zinazoonekana sehemu kubwa ya Afrika kama Trace TV, MTV BASE, Channel O na Sound City, zikaja headlines kwenye tuzo kubwa za Afrika kama MAMA Awards na sasa hii ya Brazil imefatia.

Taarifa ikufikie kwamba wimbo wa Diamond wa number 1 rmx ft. Davido umechezwa kwenye mall inayotembelewa na mamia ya watu kila siku iitwayo Morumbi ndani ya mji wa Sao Paulo ambao mpaka mwaka 2011 ulikua na wakazi zaidi ya milioni 11.

Screen Shot 2014-05-09 at 2.13.51 AMWimbo wa Diamond ulisikika kwenye spika za mall hii ambayo naambiwa ina ukubwa wa mara tatu zaidi ya Mlimani City Dar es salaam.

Ndani ya hii mall ya Morumbi naambiwa kuna studio kubwa ambayo kuna Dj maalum ambae anapiga nyimbo mbalimbali ambazo zinasikika kwenye mall nzima kupitia spika kwenye kona mbalimbali.

Screen Shot 2014-05-09 at 2.16.12 AMHaijajulikana ulifika vipi na Dj aliupata vipi ila millardayo.com inafatilia kujua ilikuaje kupitia kwa ripota wa nguvu Mtanzania Terry Sudi ambae ndio aliusikia na kushout kwa furaha kuona mbongo mwenzake anapata nafasi kwenye nchi kama Brazil japo hawaelewi kinachoimbwa.

Screen Shot 2014-05-09 at 2.16.44 AMUnataka stori kama hizi zisikupite? ungana na mimi twitter kwa kubonyeza hapa facebook na instagram

Tupia Comments