Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

AyoTV

VIDEO: Maamuzi ya Paul Makonda yamesababisha hii barabara kufikia hapa….

on

March 11 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alifanya ziara ya kutembelea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni kujionea  kero za uharibifu wa miundombinu ikiwepo barabara na kulazimika kutoa agizo kwa Manispaa ya hiyo kuhakikisha inafanya ukarabati wa maeneo yaliyoharibika ndani ya siku 14 kabla ya kuwawajibisha.

Tayari kazi imeanza na Leo March 25 Makonda aliamua kujihakikishia mpango mzima wa utekelezaji unavyofanyika katika kukarabati wa barabara hizo..

Lakini bado mkuu wa mkoa hakuonyesha kuridhishwa na kazi iliyokuwa ikiendelea na kusema>> ‘Nilitoa siku 14 ukarabati wa hii barabara uwe umekamilika, nashukuru leo nimepita na nimekuta kazi imeanza, lakini nimewataka wahusika waangalie uwezekano wa kuwa na barabara za kudumu kwa muda mrefu‘ ;-Paul Makonda

Kuna barabara pale Makumbusho wamejenga alafu wameharibu mitaro, sasa nimemtaka mkandalasi arudi haraka na arekebishe, maana wamejaza mchanga kwenye mitaro, hatuwezi kuwa na barabara zisizokuwa na mitaro, baada ya siku kumi nitarudi tena kuhakikisha kama wamekamilisha‘ ;-Paul Makonda

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Hii ndio Video ambayo Makonda alitoa maagizo hayo..

Soma na hizi

Tupia Comments