Habari za Mastaa

VIDEO: Birdman kaenda kwa hasira kwenye kituo cha Radio, kapandishiana na Watangazaji na kuondoka

on

Rapper Birdman ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa CASH MONEY records ambaye pia mchango wake upo kwenye muziki wa kina Nicki Minaj, Drake na Lil Wayne na wengine, amejikuta kwenye headlines leo baada ya kuamua kuondoka kwenye Interview ya Radio New York Marekani.

Birdman alikua mgeni kwenye show ya asubuhi THE BREAKFAST CLUB na alipoingia tu studio kabla hajakaa alianza kwa kuwaonya Watangazaji wa show hii kwamba wanatakiwa kuliheshimu jina lake na waache kumchezea.

Baada ya kukaa kwenye kiti Birdman akiwa kaambatana na watu wake akiwemo mlinzi wake, alisema anachotaka ni kwamba wanatakiwa kumuheshimu na waache kumchezea na kulichezea jina lake zaidi ya hapo hataki kuongea kitu kingine chochote.

Pamoja na Birdman kuonyesha kuwa na hasira, Watangazaji wa hii show walionekana ku-relax na walimtaka akae aongee kwenye vipaza sauti na mbele ya camera kile alichotaka kuongea, Birdman alisema angeweza kumfata mmoja wa Watangazaji hao mtaani tu lakini ameamua kuja kuongea uso kwa uso kama Mwanaume.

Imeripotiwa Birdman amekasirishwa na kitendo cha Watangazaji hawa kwenye baadhi ya show zao zilizopita kumuongelea vibaya na anaona wanalichezea jina lake bila kujali na kumpa heshima anayostahili kwa mchango wake kwenye muziki Marekani, unaweza kutazama hii video hapa chini vagi lilivyokua studio.

ULIZIKOSA STORI ZA BONGO? MASOGANGE NA BOYFRIEND MPYA? DUDUBAYA NA MSAMAHA KWA SHETTA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments