Michezo

Breaking News: Baada ya kuondoka Man Utd, Falcao arudi tena kucheza EPL

on

Miezi takribani miwili baada ya klabu ya Manchester United kuamua kutoendelea kupokea huduma za Radamel Falcao kwa kutompa mkataba wa kudumu, mchezaji huyo wa Colombia amepata timu mpya ndani ya ligi kuu ya Uingereza. 
Falcao ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Colombia, anatarajia kujiunga na Chelsea kutokea Monaco kwa mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo.

Mchezaji huyo msimu uliopita alisajiliwa na Manchester United kwa mkopo wa mwaka mmoja na endapo angewaridhisha benchi la ufundi la klabu hiyo kwa kiwango kizuri basi angesajiliwa kwa mkataba wa kudumu, hata hivyo hakufanikiwa kumshawishi Louis Van Gaal kumpa mkataba huo.

  Sasa anajiunga na Jose Mourinho, kocha ambaye amekuwa hafichi mapenzi yake mbele ya mchezaji huyo ambaye alijaribu kumsajili kwa muda mrefu bila mafanikio.

Tupia Comments