BreakingNews

Breaking News: Kituo cha Polisi kimechomwa moto na Barabara imefungwa Bunju DAR

on

unnamed

Breaking News niliyopokea muda mfupi uliopita inahusu ishu ya vurugu zilizotokea eneo la ‘Bunju A’ Dar es Salaam, barabara imefungwa na Kituo  cha Polisi kimechomwa moto na wananchi baada ya tukio la ajali ya gari kumgonga mtoto mmoja eneo hilo.

Watu wamefunga barabara, kituo cha Polisi kimechomwa moto.. kisa hasa cha watu kuamua hivyo inatokana na tukio la ajali ambapo mtoto mmoja Radhia Omary, mwanafunzi wa Shule ya Msingi kugongwa na gari.

Askari wa Kituo hicho cha Polisi wamekimbia baada ya watu wengi kuvamia Kituo hicho na kuanza kukichoma moto… watu wanadai wameamua kufanya hivyo kwa kuwa sio mara ya kwanza tukio la ajali ya aina hiyo kutokea.

Nimerekodi Breaking News @ITV, unaweza kuisikiliza kwa kuboonyeza play hapa.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments