Mix

Breaking News: Mata awasili jijini Manchester kufanyiwa vipimo vya afya

on

article-2545739-1AF2AA2D00000578-926_634x712

Mchezaji wa Juan Mata amewasili jijini Manchester katika dimba la Carrington tayari kufanyiwa vipimo na timu yake mpya ya Manchester United.

Mata amejiunga na United baada ya timu hiyo kuvunja rekodi ya ada ya usajili kwa kukubali kulipa kiasi cha paundi millioni 37 ili kupata saini ya mchezaji huyo wa kihispania. Aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United kwa kutumia helkopta aliyokodishiwa kutoka jijini London.

Wachezaji wa United Rio Ferdinand na Robin Van Persie walitumia akaunti zao za Twitter kumkaribisha kiungo huyo ambaye anategemewa kusaini mkataba wa miaka mitano huku akilipwa kiasi cha paundi 150,000 kwa wiki.

 

article-2545739-1AF2AA3100000578-343_634x575

Tupia Comments