Baraza la Ulama katika kikao chake kilichofanyika February 01 na February 02,2023 Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Multi na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir bin Ally limetengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum kama Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam kuanzia leo February 02, 2023.
Wakati huohuo Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr.Abubakar Zubeir bin Ally amemteua Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dares Salaam kuanzia leo February 02,2023.