Vilabu 12 vikubwa Ulaya vimeamua kutangaza rasmi kuanzisha michuano mpya ya European Super League, UEFA inapinga vikali michuano hiyo ambayo imepangwa kuwa inafanyika kuanzia August & May kwa kucheza nyumbani na ugenini.
Michuano hiyo itakuwa na jumla ya timu 20 zitazotengeneza makundi mawili A & B yenye timu 10, wanaomaliza nafasi tatu za juu kila Kundi wanafuzu robo fainali, nafasi ya nne na tano kucheza Play off huku fainali ikichezwa uwanja huru.
Timu tano kati ya 20 zitakuwa zinashuka kila mwaka na tano kupanda, vilabu vilivyoridhia kuunda michuano hiyo ni AC Milan, Inter, Juventus, Atletico, Barcelona, Real Madrid, Arsenal, Liverpool, Man City, Man Utd, Chelsea na Tottenham.