Club ya Yanga SC leo imetangaza rasmi kumrejesha kikosini winga wao wa zamani wa kimataiga wa Congo DR Tuisila Kisinda ambaye alikuwa akiitumikia club ya RS Berkane ya Morocco.
Kisinda anarejea Yanga SC baada ya kujiunga na RS Berkane August 13 2021 akiwa sambamba na staa wa Simba SC Clatous Chota Chama, bado Yanga hawajaweka wazi Kisinda anarudi kwa mkopo au wamemsajili jumla kwani inasemekana alisaini mkataba wa miaka mitatu na Berkane na ametumikia mwaka mmoja.
Yanga SC hadi sasa ina wachezaji zaidi ya 12 wa kigeni Fiston Mayele, Yanick Bangala, Djuma Shabani, Jesus Moloko, Djgui Diarra, Khaleed Aucho, Lazaraus Kambole, Azizi Ki, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana, Bernard Morrison, Makambo ambapo Kisinda anakuwa wa 13 hivyo Yanga SC wanatajwa kuwa watamkata Jesus Moloko au kumtoa kwa mkopo.