Kesi iliyokuwa ikiwakabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mke wake Eva Mhando, wameishinda leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo walikuwa wakituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
April 14 2016 Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu Dar es salaam imewaachia huru baada ya kuona hawana hatia kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthbitisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi na ughushaji wa nyaraka ambao inadaiwa na maafisa wa serikali kuwa kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd ilifanya hivyo ili kupewa zabuni ambayo ilitaka kupewa na bodi hiyo ya Tanesco
Mahakama imesema Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi kwamba kampuni hii ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake kwamba ipatiwe zabuni.
Mahakama Dar imemwachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Tanesco Mhando, aliyekuwa anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya pic.twitter.com/mmkgmWlyRZ
— millardayo (@millardayo) April 14, 2016
ULIIKOSA HII YA WABUNGE WATATU WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE