Michezo

BREKING: MO Dewji ajiuzulu Simba SC

on

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC MO Dewji leo amefikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba, MO amefikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya leo ya Mapinduzi Cup 1-0 dhidi ya Mtibwa.

“Ni aibu Simba kutoshinda, baada ya kulipa mishahara inayokaribia Bilioni 4 kwa mwaka, najiuzulu kama mwenyekiti wa bodi na kubakia muwekezaji, Simba Nguvu Moja, nitatia nguvu kwenye kuendeleza miundombinu na soka la vijana”>>> MODewji

Hii inakuwa ni fainali ya nne kwa Simba SC kuwahi kupoteza katika michuano ya Mapinduzi Cup kati ya 7, wakati Mtibwa Sugar hii ni fainali yao ya pili kutwaa Ubingwa kati ya sita, inadaiwa kuwa MO Dewji msimu huu hajaridhishwa na kiwango cha Simba SC kabisa ukizingatia amefanya usajili mkubwa zaidi.

VIDEO: KUMLAUMU AISHI MANULA NI KUMKOSEA HESHIMA BALAMA WA YANGA

Soma na hizi

Tupia Comments