Katika kuhakikisha Serikali inakuza uchumi kupitia sekta ya biashara baadhi ya wanafunzi kutoka chuo kikuu Mzumbe Campus kuu ya Morogoro wamepewa mafunzo maalumu yatakoyolenga kukuza Uchumi wa Taifa kupitia biashara na Taasisi mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ikiwemo kusajili Taasisi zao kwa wakala wa usajiri na Biashara BRELA.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo kwa wanafunzi na wadau mbalimbali mkurugenzi wa miliki bunifu BRELA Loy Mhando amesema zipo faida zitokanazo na baada ya kusajili Taasisi kampuni au biashara ikiwemo utambuzi wa mahitaji katika eneo husika na ukubwa wa kiwango cha biashara utakaosabisha Serikali kukuza Uchumi kupitia ulipaji wa Kodi.
Naye Afisa leseni Mkuu kutoka Brela Abas Cothema amesema licha ya watu kusajili tangu zaman uwezekano wa kuhuisha upya usajili huu utaleta faida kwa wamiliki wote wa Makampuni biashara pamoja na Taasisi mbalimbali hivyo amewataka wadau wote kujitokeza katika usajili wa biashara zao.
Miongoni mwa Wanafunzi waliofadika na Elimu hii iliyotolewa wameipongeza BRELA kwani kuhuisha ama kusajili biashara kutakufanya kujua na kutambua miliki yako katika biashara au kazi yako ili kujiepusha na migogoro ambayo huwa ikitokea ikiwemo majina ya kampuni au Taasisi kufanana.
Elimu hii imetolewa ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Mzumbe Day Entrepreneurship yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo kuanzia tarehe 21 ikiwa ni katika jitihada za kuboresha Eanafunzi kujikita katika ujasiriamali utakaowasaidia hata baada ya kutoka chuoni.