Michezo

Kocha wa Liverpool kumbe haogopi kufukuzwa !! Wakifungwa je? Kajibu haya…

on

Klabu ya Liverpool ya Uingereza Jumapili ya October 4 inacheza mchezo wake wa nane wa Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Everton, mechi ambayo ni kubwa katika jiji la Liverpool kwani inazikutanisha timu zenye upinzani mkubwa kutoka mji mmoja, inatajwa kuwa mechi hiyo huenda ikaamua hatma ya kocha wa Liverpool Brendan Rodgers.

Liverpool itashuka katika uwanja wa Goodison Park wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 30000 ikiwa na rekodi ya kucheza mechi saba, imeshinda 3, imetoka sare 2 na kufungwa 2 na ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu, rekodi hiyo inatajwa kuongeza chachu ya Brendan Rodgers kutaka kufukuzwa kama atapoteza mchezo dhidi ya Everton.

brendan-rodgers

Stori za kazi ya Brendan Rodgers kuwa mashakani kama atapoteza mchezo na wapinzani wake wa jadi Everton zilimfikia baada ya kuulizwa na waandishi vipi haogopi kufukuzwa kazi kama akipoteza mchezo dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park?

“Hapana  tutaingia uwanjani tukiwa na dhana moja tu ya kucheza vizuri na kushinda, kama tutaingia na bahati nzuri tunaweza kushinda mchezo, kuhusu suala la kufukuzwa siogopi kufukuzwa sio kwa sababu ni kiburi au nimehakikishiwa kuwa siwezi kufukuzwa. Nitafanya kadri ya uwezo wangu kuhakikisha tunashinda”>>> Brendan Rodgers

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments