Duniani

Abiria wamepona kwenye ajali ya ndege na bado wanafungua na kesi ya ajali..

on

Ikitokea unakuwa sehemu ya watu walionusurika kwenye ajali, jambo kubwa ambalo wengi wanaanza nalo ni kumshukuru MUNGU kwa kutoka salama !!

Kama uko karibu na headlines za stori za kimataifa najua utakumbuka ile ajali ya ndege ya British Airways iliyotokea uwanja wa ndege  Las Vegas Marekani wakati ndege ikijiandaa kupaa.

Taarifa nyingine toka Chicago Marekani inahusu kesi ambayo imefunguliwa kuzishtaki Kampuni mbili, GE Aviation watengenezaji wa engine ya ndege iliyopata ajali, pamoja na Boeing Company ambao ndio watengezaji wa ndege yenyewe.

777 Everett Factory K65682-02

Abiria hao 65 waliofungua kesi hiyo wamesema wanazishtaki Kampuni hizo kwa sababu walipata misukosuko wakati wa ajali hiyo ambayo ndege waliyopanda ililipuka na kushika moto kwenye engine yake moja wakati ikiwa kwenye njia ya kurukia ndege uwanja wa McCarran International Airport, September 8 2015.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments